Nenda kwa yaliyomo

Chris Sutton

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Christopher Roy Sutton (alizaliwa 10 Machi 1973) ni mchezaji wa zamani wa soka la kulipwa na kocha wa soka kutoka Uingereza. Baadaye alifanya kazi kama mchambuzi, mtoa maoni na mtangazaji wa vipindi vya soka kwenye televisheni na redio.

Sutton alicheza soka kuanzia mwaka 1991 hadi 2007 katika klabu za Norwich City, Blackburn Rovers, Chelsea, Celtic, Birmingham City na Aston Villa.

Katika kipindi cha miaka 16 ya uchezaji wake katika Premier League ya Uingereza na Premier League ya Scotland, Sutton alifunga zaidi ya mabao 150 katika zaidi ya mechi 400 za ligi.

Maisha ya Awali

[hariri | hariri chanzo]

Chris Sutton alizaliwa tarehe 10 Machi 1973 katika jiji la Nottingham, eneo la East Midlands, nchini Uingereza. Alikuwa mtoto wa Mike Sutton, ambaye hapo awali alikuwa mchezaji wa soka wa Norwich City.

Kaka yake mdogo, John Sutton, pia alifuata nyayo za baba na kaka yake na kuwa mchezaji wa soka. John amechezea klabu mbalimbali nchini Uingereza na Scotland.

Akiwa mtoto, Chris Sutton alihama pamoja na familia yake kutoka East Leake, katika kaunti ya Nottinghamshire, na kwenda Horsford, katika kaunti ya Norfolk.[1][2]

  1. ↑ https://www.soccerbase.com/players/player.sd?player_id=7732
  2. ↑ https://www.sporting-heroes.net/football/
Image Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chris Sutton kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.