Nenda kwa yaliyomo

Elementi sintetiki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Elementi sintetiki ni elementi za kikemia ambazo hazitokei kiasili duniani bali zinaweza kutengenezwa katika maabara. Zinaitwa pia transurania kwa sababu ziko nzito kushinda urani ambayo ni elementi nzito zaidi inayopatikana duniani kiasili.

Hazipo kiasili kwa sababu si imara kutokana na nusumaisha fupi mno; kama zilipatikana kutokana na mmenyuko wa kinyuklia asilia, zilipotea tayari tangu muda mrefu.

Muda wa maisha ya elementi sintetiki ni kati ya sekunde (au sehemu za sekunde tu) hadi miaka kadhaa. Zote ni nururifu yaani zinatoa mnururisho wa kinyuklia.

Orodha ya elementi sintetiki

[hariri | hariri chanzo]

Elementi zifuatazo hazitokei kiasili duniani. Zote ni transurania zikiwa na namba atomia kuanzia 95 kwenda juu.

Jina la elementiAlamaNamba
atomia
Kuwepo ilithebitishwa
mara ya kwanza
AmerikiAm951944
KuriCm961944
BerkeliBk971949
CaliforniumCf981950
EinsteiniEs991952
FermiFm1001952
MendeleviMd1011955
NobeliNo1021966
LawrenciLr1031971
RutherfordiRf1041966 (USSR), 1969 (U.S.) *
DubniDb1051968 (USSR), 1970 (U.S.) *
SeaborgiSg1061974
BohriBh1071981
HassiHs1081984
MeitneriMt1091982
DarmstadtiDs1101994
RoentgeniRg1111994
KopernikiCn1121996
NihoniNh1132004
FleroviFl1142004
MoskoviMc1152010
LivermoriLv1162004
TennessiniTs1172010
OganessiOg1182006
* imethebitishwa mwaka uleule