Nenda kwa yaliyomo

Lady Jay Dee

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lady Jay Dee
Jide akiwa katika pozi
Jide akiwa katika pozi
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Judith Daines Wambura Mbibo
Pia anajulikana kama Binti Machozi
Komandoo
Jidee
Jay Dee
Amezaliwa 6 Juni 1979 (1979-06-06) (umri 46)
Asili yake Mkurya
Aina ya muziki R&B
Bongo Flava
Afro-Pop
Kazi yake Mwanamuziki
Ala Sauti
Miaka ya kazi 1999-hadi leo
Studio MJ Records
FM Studio
Bakunde Production
Ame/Wameshirikiana na Mr. II
Professor Jay
Juma Nature
Inspector Haroun
Q. Chillah
Mwana FA

Judith Daines Wambura Mbibo (anafahamika zaidi kwa jina la kisanii kama Lady Jay Dee; amezaliwa mkoani Shinyanga 15 Juni 1979) ni mwanamuziki wa Bongo Flava-Afro pop kutoka nchini Tanzania[1].

Maisha ya awali

Judith Wambura alizaliwa na Martha na Lameck Isambua Mbibo ambao ndio wazazi wake. Alianza kuimba akiwa na umri wa miaka saba. Alianzia kuimba kanisani kama ilivyo kwa wasanii wengi. Baada ya kumaliza shule, Lady Jaydee aliwahi kufanya kazi Clouds FM kabla ya kuamua kujiingiza kwenye masuala ya muziki hapo mnamo miaka ya 2000.[2]

Ushirikiano wa Kibiashara

  • Mnamo mwaka 2009, alisaini mkataba na Zain Tanzania (ambayo sasa inajulikana kama Airtel Tanzania) kuwa balozi wao.
  • Mnamo mwaka 2010, aliteuliwa na Comprehensive Community Based Rehabilitation In Tanzania (CCBRT) kuwa balozi wao kwa ajili ya kusaidia wanawake wanaosumbuliwa na ugonjwa wa fistula.
  • Mnamo mwaka 2012, alikuwa balozi wa NMB (National Microfinance Bank) Tanzania katika mradi uliofahamika kama "PESA FASTA".
  • Mnamo Machi 2014, alisaini mkataba na kampuni ya kimataifa ya vipodozi Oriflame Sweden kuwa mmoja wa mabalozi wa chapa hiyo.
  • Mnamo mwaka 2014, aliteuliwa na Marie Stopes Tanzania kuwa Balozi wa Uzazi wa Mpango Tanzania.
  • Mnamo Juni 2015, alisaini mkataba na mgodi wa dhahabu wa Geita (Geita Gold Mine) kuwa Balozi wa Mfuko wa Changamoto wa Geita Gold Mine dhidi ya VVU/UKIMWI.

Shughuli za muziki

Alianza kujibebea heshima katika medani ya muziki kunako mwaka wa 2000 baada ya kutoa albamu yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la "Machozi" na kutoa single kadhaa kutoka katika albamu hiyo na kumfanya kuwa mwanamama wa kwanza katika bongo flava kwa kutumia gharama kubwa ya ujenzi wa albamu katika historia ya muziki wa kizazi kipya.

Lady Jay Dee ni msanii mwenye kumiliki studio yake mwenyewe ya kurekodia. Studio inakwenda kwa jina la Jag Records.

Jay Dee, alishawahi kuchaguliwa kuwa Mwanamuziki Bora wa Kike wa Tanzania kwa muziki wa R&B mnamo 2002, na kutumbuiza katika Kora All Africa Designers Competition, na kutuzwa "Albamu Bora ya R&B" katika Tuzo za Muziki Tanzania kunako tar. 6 Agosti 2004. Kunako mwezi wa Julai 2005, ameshinda tuzo ya "video bora ya msanii wa kike kwa Afrika Kusini".

Muziki

Albamu zake

Jay Dee, ametoa albamu saba za muziki:

Marejeo

  1. https://www.jamiiforums.com/threads/historia-ya-lady-jaydee.522321/
  2. "Manka kwenye BC". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-11-05. Iliwekwa mnamo 2009-10-13.

Viungo vya Nje

Image Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani wa Afrika bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lady Jay Dee kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.