Warren G
| Warren G | |
|---|---|
Warren G mnamo mwaka 2015 | |
| Taarifa za awali | |
| Jina la kuzaliwa | Warren Griffin III |
| Amezaliwa | 10 Novemba 1970 |
| Chimbuko | Long Beach, California, Marekani |
| Aina ya muziki | West Coast hip-hop G-funk |
| Kazi yake | Rapa mwandishi wa nyimbo mtayarishaji wa rekodi DJ muigizaji |
| Miaka ya kazi | 1990–sasa |
| Studio | G-Funk Violator RAL Def Jam |
| Ameshirikiana na | 213 Nate Dogg Snoop Dogg Dr. Dre |
| Wavuti | warreng.com |
Warren Griffin III (alizaliwa Novemba 10, 1970)[1] ni rapa, mtayarishaji wa rekodi, na DJ kutoka nchini Marekani. Anajulikana sana kwa mchango wake katika kutangaza na kueneza muziki wa West Coast hip hop mnamo miaka ya 1990, na anatambulika kama mmoja wa waanzilishi wa mtindo mdogo wa rap unaojulikana kama G-funk.[2]
Griffin alipata mafanikio makubwa kibiashara mnamo mwaka 1994 kupitia wimbo wake wa "Regulate" (akimshirikisha Nate Dogg), ambao ulishika nafasi ya pili kwenye chati za Billboard Hot 100. Albamu yake ya kwanza, Regulate... G Funk Era (1994), ilianza katika nafasi ya pili kwenye chati ya Marekani ya Billboard 200, ikiuza nakala 176,000 katika wiki yake ya kwanza. Tangu wakati huo, imetunukiwa cheti cha Platinamu mara tatu na chama cha Recording Industry Association of America (RIAA), ikimaanisha imeuza nakala milioni tatu. Wimbo wa "Regulate" ulikaa kwa wiki 18 kwenye orodha ya nyimbo 40 bora za Billboard Hot 100, huku ukishika nafasi ya pili kwa wiki tatu, wakati wimbo uliofuata wa "This D.J." ulishika nafasi ya tisa. Kwenye usiku wa utoaji wa Tuzo za 37 za Kila Mwaka za Grammy, nyimbo zote mbili zilipata uteuzi wa Utendaji Bora wa Rap wa Kundi au Wawili na Utendaji Bora wa Solo wa Rap.
Nyimbo tatu kutoka kwenye albamu yake ya pili, Take a Look Over Your Shoulder (1997), ziliingia kwenye 40 bora, kama ilivyokuwa kwa wimbo wake wa ushirikiano wa mwaka 1998 na Nate Dogg uitwao "Nobody Does It Better". Albamu hiyo pamoja na ile iliyofuata ya I Want It All (1999), zote zilipata mauzo ya Dhahabu kutoka RIAA. Albamu yake ya nne, The Return of the Regulator (2001), haikupata mafanikio makubwa sana. Akishirikiana na washikaji zake wa zamani Snoop Dogg na Nate Dogg, walilounda kundi la hip-hop la watatu liitwalo 213, lililopewa jina kufuatia msimbo wa eneo la Long Beach, California; walitoa albamu ya The Hard Way (2004) ambayo ilipata mafanikio ya wastani. Albamu zake mbili zilizofuata, In the Mid-Nite Hour (2005) na The G Files (2009), zilitolewa kijitegemea na alizitayarisha yeye mwenyewe.
Anasifika pia kwa kuwa mtu aliyemgundua Snoop Dogg, baada ya kumtambulisha rapa huyo kwa mtayarishaji wa rekodi Dr. Dre. Mnamo mwaka 2015, alitoa albamu fupi (EP) ya Regulate... G Funk Era, Part II, iliyojumuisha sauti za kumbukumbu za Nate Dogg, aliyefariki dunia mnamo mwaka 2011.
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Warren Griffin III alizaliwa mnamo Novemba 10, 1970, na alikulia huko Long Beach, California.[1] Ana dada watatu huku akiwa mtoto pekee wa kiume wa Warren Griffin Jr., ambaye alikuwa fundi wa ndege, na Ola, ambaye alikuwa mtaalamu wa lishe.[1] Wazazi wake walitengana wakati Griffin akiwa na umri wa miaka minne, na akaishi na mama yake pamoja na dada zake watatu huko East Long Beach.[1]
Mnamo mwaka 1982, Griffin alihamia kuishi na baba yake huko North Long Beach.[1] Mama yake wa kambo, Verna, alikuwa na watoto watatu kutoka kwenye ndoa yake ya nyuma,[1] na mmoja wao alikuwa Andre Young (Dr. Dre), ambaye katikati ya miaka ya 1980 alikuwa mwnachama wa kundi la muziki wa electro-rap la World Class Wreckin' Cru, ambalo mnamo mwaka 1987 lilitoa rekodi ya kwanza ya rap ya eneo la Los Angeles chini ya lebo kubwa ya muziki.[3][4] Griffin alisoma katika Shule ya Sekondari ya Jordan na alicheza mchezo wa soka la Kimarekani.[1][5]
Mnamo mwaka 1988, Griffin alifungwa jela akiwa na umri wa miaka 17 kwa kosa la kumiliki silaha.[1] Akiwa gerezani, alichagua jina la utani la Warren G.[1] Kufikia kipindi hiki, Dr. Dre alikuwa tayari ameshaanza kupata mafanikio makubwa kama mwandishi na mtayarishaji wa rekodi wa lebo ya Ruthless Records, na pia akiwa mwanachama wa kundi la N.W.A akishirikiana na mwanzilishi wa Ruthless Records Eazy-E pamoja na Ice Cube. Albamu ya kihistoria ya N.W.A, Straight Outta Compton (1989), ilikuwa ikisababisha mapinduzi makubwa kwenye tasnia ya rap ya Los Angeles kwa kuachana na mtindo wa electro na kuingia rasmi kwenye gangsta rap.[4] Baada ya kuachiliwa kwake, Griffin alifanya kazi katika jumba la uundaji wa meli wa Long Beach[1][6] na kuanza kujikita zaidi kwenye muziki baada ya Dr. Dre kumfundisha jinsi ya kutumia mashine ya midundo (drum machine).[1]
Kufikia mwaka 1990, Warren G alikuwa ameshaunda kundi la watatu la 213[7] akishirikiana na washikaji zake wawili wa muda mrefu, Nate Dogg na Snoop Dogg. Kundi la 213 lilikuwa mchangiaji mkubwa wa mtindo wa G-funk ambao ulikuwa unakaribia kuibuka kwenye muziki wa rap.[8] Kundi hilo lilivunjika baada ya Warren G kuwakutanisha na Dr. Dre. Katika hatua hiyo, kazi za peke zao za Dr. Dre na Snoop Dogg zilizinduliwa rasmi kupitia misingi ya G-funk.[9] Nate Dogg naye alisajiliwa kwenye lebo ya Dr. Dre ya Death Row Records.[9] Warren G mwanzoni alisaidia kazi hapo; hata hivyo, kwa kutofikiria kufanya kazi chini ya kivuli cha kaka yake wa kambo na mshauri wake, aliamua kusaini mkataba na lebo ya Def Jam Recordings iliyopo jijini New York City.[1][10]
Diskografia
[hariri | hariri chanzo]Albamu za studio
- Regulate... G Funk Era (1994)
- Take a Look Over Your Shoulder (1997)
- I Want It All (1999)
- The Return of the Regulator (2001)
- In the Mid-Nite Hour (2005)
- The G Files (2009)
Albamu za ushirikiano
- The Hard Way (akishirikiana na 213) (2004)
Filmografia
[hariri | hariri chanzo]- The Show (1995)
- Speedway Junky (1999)
- Little Richard (2000)
- The Parkers (2000)
- Old School (2003)
- All of Us (2005)
- BTS American Hustle Life (2014)
- The Eric Andre Show (2016), sehemu 1
Michezo ya video
[hariri | hariri chanzo]- Rap Jam: Volume One (1995)
- Def Jam: Fight for NY (2004)
- Def Jam Fight for NY: The Takeover (2006)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 Brenna Sanchez, "Contemporary Musicians: Warren G", Encyclopedia.com, Cengage, updated April 12, 2020.
- ↑ Steve Huey, "Warren G: Biography", AllMusic.com, Netaktion LLC, visited May 8, 2020.
- ↑ David Diallo, ch 10 "From electro-rap to G-funk: A social history of rap music in Los Angeles and Compton, California", in Mickey Hess, ed., Hip Hop in America: A Regional Guide, Volume 1: East Coast and West Coast (Westport, CT: Greenwood Press, 2010).
- 1 2 David Diallo, "Dr. Dre and Snoop Dogg", in Mickey Hess, ed., Icons of Hip Hop: An Encyclopedia of the Movement, Music, and Culture (Santa Barbara, CA: Greenwood Press, 2007), pp 319–322.
- ↑ "Jordan High School Class of 1997". jordanhighschool.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-12-15. Iliwekwa mnamo 2024-12-15.
- ↑ "Warren G". Hip Hop Scriptures (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-12-15.
- ↑ Mosi Reeves, "Warren G and Nate Dogg's 'Regulate': The oral history of a hip-hop classic", Rolling Stone website, Penske Media LLC, December 19, 2014.
- ↑ Jeff Weiss anaeleza, "Kama vile The Chronic ilivyo mabadiliko ya kisaikolojia na ya kichawi kutoka kwenye rekodi za Parliament na Funkadelic zilizokuwa zikizunguka kila mara kwenye mtambo wa Dre tangu utotoni, pia ni sauti ya Long Beach: nyimbo za kikanisa za Baptist zilizobadilishwa kuwa harmonic gospel chafu na Snoop, Nate Dogg, Warren G na Daz."
- 1 2 Ben Westhoff, "The making of The Chronic", LA Weekly, November 19, 2012.
- ↑ Hitilafu ya kutaja: Invalid
<ref>tag; no text was provided for refs named ":23".
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]